• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi wa Marekani watumia virusi vya Zika kutibu saratani ya ubongo

    (GMT+08:00) 2017-10-10 08:20:29

    Ingawa virusi vya Zika vinaweza kuharibu ubongo wa watoto wachanga na kusababisha ugonjwa wa kichwa kidogo, lakini utafiti mpya uliofanywa na Marekani umeonesha kuwa iko siku virusi hivyo vitaweza kutibu saratani ya ubongo.

    Watafiti wa Chuo cha San Diego cha Chuo Kikuu cha California na chuo cha matibabu cha chuo kikuu cha Washington wamesema, waliingiza virusi vya Zika katika sampuli za saratani ya ubongo, baada ya siku saba virusi hivyo viligunduliwa kukua na kuzuia ukuaji wa seli za saratani.

    Juu ya msingi wa ugunduzi huo, watafiti walijaribu kutumia virusi vya Zika kutibu panya waliopata saratani ya ubongo. Baada ya wiki mbili, uvimbe wa panya hao unakuwa mdogo zaidi ukilinganishwa na wa panya wasiopata tiba hiyo, ambao hatimaye wanaishi maisha marefu zaidi.

    Watafiti wanaona kuwa, tiba ya virusi vya Zika na tiba iliyokuwepo hivi sasa zitaunganishwa pamoja. Katika siku za baadaye, virusi vya Zika vitawekwa ndani ya ubongo wa wagonjwa. Virusi hivyo vinaweza kuharibu seli za mfumo wa neva wa watoto wachanga, lakini havitaleta athari mbaya kwa watu wazima.

    Watafiti wa Marekani pia wamesisitiza kuwa, hali ya virusi vya Zika katika mwili wa binadamu inaweza kuwa tofauti na ile katika mwili wa panya. Hivyo tiba hiyo itafanyiwa majaribio mengi zaidi katika siku za baadaye, ili kuthibitisha usalama na mchango wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako