• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanyama wakubwa zaidi na wadogo zaidi wenye uti wa mgongo wana uwezekano mkubwa zaidi wa kutoweka

    (GMT+08:00) 2017-10-10 21:04:24

    Kikundi cha watafiti kutoka Australia, Marekani na Uswisi kimetoa ripoti kwenye gazeti la PNAS la Marekani ikisema wamechambua data za wanyama wenye uti wa mgongo zaidi ya aina elfu 27 ili kutafiti uwezekano wao wa kutoweka.

    Matokeo yanaonesha kuwa wanyama wenye ukubwa na uzito mkubwa zaidi na wale wenye mdogo zaidi wote wana hatari kubwa ya kutoweka. Tofauti kati yao ni kwamba wale wakubwa wanakabiliwa na tishio la kuwindwa na binadamu, na wale wadogo wanakabiliwa na uchafuzi na kupungua kwa makazi kutokana na kilimo na ukataji wa misitu.

    Watafiti wamesema kutoweka kwa papa nyangumi, mjusi mkubwa aina ya Komodo Dragon na popo mwenye pua zinazofanana na nguruwe kutaleta hasara kubwa kwa mazingira ya viumbe, na watu wanatakiwa kuchukua hatua kuwahifadhi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako