• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema gharama za juu zazuia biashara na uwekezaji wa moja kwa moja

    (GMT+08:00) 2017-10-11 09:14:02

    Gharama kubwa za uwezeshaji wa biashara na huduma mbaya za vifaa ni kikwazo katika uwekezaji wa moja kwa moja na ukuaji katika kanda ya Afrika Mashariki.

    Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu wa biashara wa Kenya Chris Kiptoo kwenye uzinduzi wa ripoti ya utafiti juu ya ufanisi wa vifaa ya mwaka 2017 huko mjini Nairobi. Amesema vifaa vizuri sio tu vinapunguza gharama za uagizaji, na pia ni muhimu kwa wazalishaji kuweza kushiriki kwenye mzunguko wa uzalishaji duniani na hatimaye kuingia kwenye biashara mpya.

    Ripoti hiyo iliyotolewa na Shippers Council of East Africa (SCEA), imesema mazingira ya uendeshaji wa biashara yameboreka kutokana na uchaguzi sahihi wa sera, kuongezeka kwa biashara ya ndani ya kanda, na kuwezesha sekta binafsi. Pia imechambua ufanisi wa vifaa vya biashara sambamba na viashiria vya muda, gharama na ugumu ikilinganisha na vituo vya biashara vinavyoongoza duniani, na kuonesha kuwa mageuzi yaliyoanzishwa na nchi wajumbe yanaanza kuzaa matunda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako