• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Simba Sports Club, Stand United zapigwa faini

  (GMT+08:00) 2017-10-11 09:26:06

  Kamati ya bodi ya ligi ya uendeshaji na usimamizi wa ligi imezitwanga faini ya Sh 500,000 kila moja klabu za Simba ya Dar es salaam na Stand United ya Shinyanga.

  Klabu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na wachezaji wake kuvaa jezi zenye namba tofauti na zile zilizosajiliwa, na faini ya shilingi 500,000 kutokana na mashabiki wa timu hiyo kuingia uwanjani kushangilia ushindi baada ya mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyofanyika Septemba 23 mwaka huu uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

  Klabu ya Simba yenyewe wamepewa adhabu ya faini ya shilingi 500,000 kutokana na timu yake kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Septemba 21 mwaka huu uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako