• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kuboreshwa kwa mazingira ya biashara nchini China kunazinufaisha kampuni za nchi za nje

  (GMT+08:00) 2017-10-11 18:09:54

  Wakurugenzi wa kampuni nyingi za nchi za nje nchini China hivi karibuni walipohojiwa na waandishi wa habari wa Redio China Kimataifa walisema, katika miaka mitano iliyopita kampuni zao zimeona mabadiliko mazuri ya soko la China, pia zimenufaika na sera husika za China. Kutokana na utekelezaji wa pendekeo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na mpango wa "Made in China 2025", kampuni hizo zina imani kubwa na mustakabali wa soko na uchumi wa China.

  Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya GE Bi. Duan Xiaoying alisema, mazingira ya biashara nchini China yanaboreshwa siku hadi siku, na idara za serikali za ngazi mbalimbali nchini humo zinarahisisha zaidi mambo ya kiserikali, na zimejenga utaratibu mfululizo wa kuzihudumia kampuni, hii inazisaidia kampuni kupunguza gharama za biashara na kuinua kiwango cha ufanisi.

  Bi. Duan Xiaoying amesema, tangu eneo la biashara huria la Shanghai lianzishwe mwaka 2013, kampuni ya GE imeona urahisi wa sera kwenye usimamizi wa viwanda na biashara, forodha, na ukaguzi wa biashara. Amesema ikilinganishwa na zamani, idara husika zimefupisha muda wa kushughulikia mambo, pia zimepanga watu maalumu wa kutatua masuala fulani.

  Katika miaka 5 iliyopita, China imetangaza sera na hatua mfululizo, ili kuongeza ruhusa ya uwekezaji wa nje, na kuweka mazingira ya usawa ya ushindani. Mwezi Januari mwaka huu, Baraza la serikali ya China lilitangaza hatua 20 za kuvutia uwekezaji wa kigeni, ambazo ni pamoja na kuongeza zaidi ruhusa ya uwekezaji wa nchi za nje kwenye sekta za huduma, utengenezaji, na uchimbaji wa madini, na kuziunga mkono kampuni za nchi za nje kunufaika na mkakati wa "Made in China 2025" pamoja na kampuni za China.

  Kwa mujibu wa ripoti iliyotolwa na Benki ya Dunia kuhusu mazingira ya biashara duniani mwaka 2017, kiwango cha urahisi wa biashara nchini China kiliinuka kwa nafasi 18 katika miaka 3 iliyopita.

  Meneja mkuu wa kampuni ya Kollmorgen nchini China Bw. Liu Weifeng amesema, katika miaka kadhaa iliyopita, mazingira ya utawala wa kisheria nchini China yameboreshwa zaidi, na kampuni za nchi za nje zinaweza kuingia kwenye ushindani katika mazingira ya haki na usawa zaidi. Vilevile amesema serikali za mitaa zimeongeza nguvu za kuziunga mkono kampuni. Bw. Liu amesema serikali za mitaa na vyuo vikuu vingi zaidi vimeeleza matumaini ya kufanya ushirikiano na kampuni za nchi za nje.

  Kampuni ya MasterCard ambayo imeingia kwenye soko la China kwa miaka 31 imeshuhudia maendeleo ya kasi ya uchumi wa China, pia imeleta urahisi mkubwa kwa wateja wa China. Mkurugenzi wa kampuni ya MasterCard nchini China Bw. Chang Qing amesema, China ni soko muhimu zaidi duniani la MasterCard.

  Bw. Chang amesema, miaka 5 iliyopita ni muda wa maendeleo makubwa kwa kampuni ya MasterCard. Kampuni ya MasterCard imefanya ushirikiano na benki zaidi ya 40 za China, na kutoa huduma mpya za aina zaidi ya mia moja.

  Uchunguzi uliofanywa na Mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa pia unaonesha kuwa, China bado ni soko linalovutia kampuni za nchi za nje.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako