• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kuyasikia bombani mashindano ya dunia

    (GMT+08:00) 2017-10-12 09:03:27

    Marekani hawatashiriki michuano ya Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi baada ya kulazwa kwa mabao 2-1 na Trinidad & Tobago kwenye mechi ya kufuzu michuano hiyo.

    Panama walikitia mchanga kitumbua cha Marekani kwa kuandikisha ushindi dhidi ya Costa Rica. Vijana hao wa Bruce Arena walianza mechi wakiwa katika nafasi ya tatu ya kufuzu kwa Kombe la Dunia lakini bao la ushindi la Roman Torres dakika ya 88 liliwafikisha Panama kwa michuano hiyo kwa mara ya kwanza. Marekani hawakupata hata nafasi ya kucheza michuano ya muondoano ya kufuzu dhidi ya Australia, kwani nafasi hiyo iliwaendea Honduras waliowalaza Mexico.

    Mara ya mwisho Marekani kukosa kushiriki fainali za Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1986. Marekani waliilaza Panama mabao 4-0 Ijumaa iliyopita lakini licha ya kucheza dhidi ya Trinidad & Tobago waliokuwa na alama tatu pekee katika mechi tisa walizocheza awali za kufuzu, walicheza vibaya sana na hakukuwa na matumaini ya kushinda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako