• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya dunia yasema eneo la Afrika Kusini mwa Sahara kuwa na ongezeko zuri la uchumi kwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-10-12 09:25:35

    Benki ya dunia imekadiria kuwa eneo la Afrika Kusini mwa sahara litakuwa na ongezeko la kuridhisha la ukuaji wa uchumi la asilimia 2.4 kwa mwaka 2017, ikilinganishwa na asilimia 1.3 ya mwaka jana.

    Hata hiyo kwenye ripoti mpya inayotolewa mara mbili kwa mwaka kuhusu uchambuzi wa mwenendo wa uchumi wa nchi za Afrika, benki ya dunia imetahadharisha kuwa kasi ya kufufuka kwa uchumi wa eneo hilo itaendelea kuwa ya kulegalega, na haitatosha kuinua kiwango cha mapato ya watu.

    Mchumi mkuu wa Benki ya dunia kanda ya Afrika Bw Albert Zuefack, amesema nchi nyingi za Afrika hazina wigo mpana wa hatua ya kifedha kukabiliana na kuyumba kwa hali ya uchumi.

    Amesema ni muhimu kwa nchi za Afrika kufuata sera sahihi na hatua za kimuundo, ili kuimarisha uwezo wa uchumi kuhimili mabadiliko, kuhimiza uzalishaji, kuongeza uwekezaji na kuwa na vyanzo mbalimbali vya mapato.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako