Tarehe 30 mwezi Machi mwaka 2013, rais Xi Jinping wa China aliyefanya ziara nchini Jamhuri ya Congo, yeye pamoja na mwenyeji wake rais Denis Sassou-Nguesso walishiriki kwenye sherehe ya kuzinduliwa kwa maktaba ya Chuo Kikuu cha Marien Ngouabi iliyojengwa kwa msaada wa China. Rasi Xi pia alifanya mazungumzo na mwalimu wa chuo cha Confucius Bi. Ai Jia. Hivi sasa ni miaka 4 imepita tangu rais Xi afanye ziara hiyo, lakini Bi. Ai Jia bado anakumbuka hali ya wakati ule.
Ai Jia ni jina la Kichina la Bi Edwige Kamitewoko, ambaye alisoma katika Chuo kikuu cha Zhejiang nchini China kwa miaka minne, na baada ya kuhitimu kutoka Chuo kikuu cha Zhejiang, amekuwa mwalimu wa chuo cha uchumi na chuo cha Confucius katika Chuo kikuu cha Marien Ngouabi. Bibi Ai anakumbuka vizuri hali ya kukutana na marais hao wawili mwaka 2013, Anasema,
"Jambo hilo liliniachia kumbukumbu nzuri. Wakati ule nilikuwa ninafurahi sana. Rais Xi Jinping aliniuliza nilijifunza lugha ya Kichina wapi. Nilimjibu Hangzhou. Aliendelea kuniuliza lini, nilijibu ni kuanzia mwaka 2001 hadi 2005. Aliniuliza kama naupenda mji wa Hangzhou au la, nilijibu kuwa naupenda sana, kwani Hangzhou ni mji mzuri. Alisema wakati ule yeye alikuwa anafanya kazi mjini Hangzhou, lakini hatukufahamiana."
Bibi Ai Jia bado anahifadhi video na picha kuhusu kufanya mazungumzo na marais wawili. Anasema,
"Rais Xi Jinping aliniuliza kama walimu wa chuo cha Confucius wanatoka China au Congo. Nilisema walimu wawili wa China wamewasili chuoni, na mimi ni mwalimu pekee mwenyeji. Rais Xi alisifu nguvu ya walimu ya chuo cha Confucius. Rais Sassou pia aliniuliza lini nilianza kufundisha wanafunzi lugha ya Kichina, nilijibu nimefundisha kwa miaka sita. Rais Sassou alifurahi sana, na alinihimiza kuendelea na kazi yangu."
Hivi sasa, licha ya kufundisha wanafunzi elimu ya uchumi na lugha ya Kichina, Bi. Ai Jia pia ni mkurugenzi wa idara ya kazi na uhusiano wa kimataifa ya Chuo kikuu cha Marien Ngouabi, ambaye anafuatilia sana habari za kimataifa kuhusu China. Ameona kuwa kwa uongozi wa rais Xi Jinping, China imepata mafanikio makubwa yanayoishangaza dunia. Anasema,
"Rais Xi Jinping ni kiongozi mwenye imani kubwa, anayeshughulikia mambo kwa makini. Mtazamo wake ni sahihi, hivyo napenda sana uongozi wake. Hivi sasa maendeleo ya China yanafuatiliwa na dunia, hata yamekuwa nguzo ya kukuza uchumi. Tunapaswa kuiga uzoefu wa maendeleo ya China, na kuiendeleza Jamhuri ya Congo kwa mujibu wa njia yamaendeleo ya China."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |