• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Namibia yathibitisha viboko na nyati wengi wamekufa kutokana na maambukizi ya Anthrax

    (GMT+08:00) 2017-10-12 18:45:55

    Wizara ya mazingira na utalii ya Namibia imethibitisha kuwa kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 10 mwezi huu, viboko 12 na nyati 25 walikufa kutokana na maambukizi ya Anthrax katika hifadhi ya kitaifa ya Bwabwata.

    Taarifa ya wizara hiyo imesema, wataalamu wa wanyamapori na idara ya matibabu ya wanyama ya wizara ya kilimo wanaendelea na uchunguzi, na kuchukua hatua ili kuzuia kuongezeka kwa vifo vya wanyama.

    Wizara hiyo imewaonya wakazi wasiguse au kula miili ya wanyama walioambukizwa, ili wasiathiriwe vibaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako