• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa PSG Nasser Al Khelaifi aingia kwenye kashfa ya rushwa

  (GMT+08:00) 2017-10-13 08:38:22

  Tajiri wa Qatar ambaye ni raisi wa klabu ya PSG Nasser Al Khelaifi ameingia katika kesi ya rushwa kwa kudaiwa kutoa kiasi kikubwa cha pesa kwa mmoja wa maafisa wa FIFA ili kupewa haki za matangazo. Al Khelaifi ambaye majuzi tu aliishangaza dunia kwa kufanya usajili uliovunja rekodi ya dunia kumnunua Neymar anadaiwa kwamba alihitaji kumiliki haki za kurusha matangazo ya michezo ya kombe la dunia mwaka 2026 na 2030.

  Jerome Vackle aliyekuwa secretary wa zamani wa chama cha soka duniani FIFA anadaiwa alipewa kiasi cha pesa kwa ajili ya kulisaidia shirika la Bein Sports kupata haki za matangazo hayo ya kombe la dunia.

  Kuhusishwa kwa Al Khelaifi na kesi hii kunazidi kuiweka Qatar karibu na kashfa ya rushwa katika fainali za kombe la dunia 2022 ambapo kesi ya Vackle naye ambaye alitimuliwa na FIFA kutokana na kesi za rushwa anazidi kuchafuka. Maofisa wa masuala ya rushwa kutoka Uswisi wamesema El Khelaifi ambaye ni bosi wa shirika la Bein Sports alilitumia shirika lake kama njia ya kupata tenda hiyo ya matangazo ya kombe la dunia na tayari maofisa hao wameanza uchunguzi dhidi ya Al Khelaifi. Bado hadi sasa raisi huyo wa PSG hajazungumza lolote juu ya madai dhidi yake japo hii inaweza kuwa kesi kubwa itakayomchafua yeye pamoja na Qatar kuelekea fainali za kombe la dunia mwaka 2022.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako