• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wajumbe wa Umoja wa Ulaya wasema hakuna maendeleo yaliyopatikana kwenye duru ya tano ya mazungumzo ya Brexit

  (GMT+08:00) 2017-10-13 09:22:53

  Duru ya tano ya maungumzo ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya imemalizika jana mjini Brussels, Ubelgiji.

  Mwakilishi wa Uingereza anayeshughulikia mambo ya Brexit Bw David Davies amesema maendeleo yamepatikana kwenye mazungumzo hayo, kauli inayopingwa na mjumbe mkuu wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw Michel Barnier, akisema kuwa malipo ya Brexit bado ni suala kuu linalojadiliwa, na kwamba mazungumzo hayo bado hayajaanza kugusa mambo halisi.

  Malipo hayo ni pamoja na mishahara ya wafanyakazi wastaafu wa zamani wa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, malipo ya mashirika ya Umoja wa Ulaya yaliyohamia nchini Uingereza, na ahadi husika kwa ajili ya mambo ya kifedha ya Umoja wa Ulaya.

  Inakadiriwa kwamba idadi ya malipo ya Brexit ingefikia paundi bilioni 50 hadi bilioni 100, sawa na dola bilioni 66 hadi bilioni 132 za kimarekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako