• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi wa kituo cha kuwaokoa wanyama pori nchini Zimbabwe amsifu rais Xi Jinping wa China kwa nia yake ya kuwahifadhi wanyama

    (GMT+08:00) 2017-10-13 18:19:36

    Mwishoni mwa mwaka 2015 rais Xi Jinping wa China na mke wake walipofanya ziara nchini Zimbabwe walitembelea kituo cha kuwaokoa wanyama pori nchini humo. Hii ni mara ya kwanza kwa kituo hicho chenye historia ya miaka 20 hivi kutembelewa na kiongozi wa nchi ya nje. Mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Roxy Danckwerts alipokumbuka kukutana na rais Xi Jinping, alisema rais Xi ni mtu mwenye nia halisi ya kuhifadhi wanyama.

    Bi. Roxy amesema, wakati wafanyakazi wote walipoambiwa rais Xi Jinping wa China atakwenda kwenye kituo hicho, walifurahi sana. Alianza kuangalia habari kuhusu rais Xi kwenye mtandao wa Internet. Alielewa kabla ya hapo rais Xi Jinping alifikia maoni ya pamoja na rais Barack Obama wa Marekani kuhusu kusitisha biashara ya pembe za ndovu, hivyo alitaka kufanya mazungumzo na rais Xi kuhusu kuhifadhi wanyama, lakini alitumai mazungumzo hayo yatakuwa rasmi .

    Alipokuwa akinywa chai kwenye kituo cha kuwaokoa wanyama pori, rais Xi Jinping na mke wake Bi. Peng Liyuan pamoja na familia ya Bi. Roxy walifanya mazungumzo. Bi. Roxy alitambua rais Xi na mke wake ni watu wazuri, na ni furaha kubwa kuzungumza nao.

       Bi. Roxy alisema, walijadiliana kuhusu uhifadhi wa wanyama. Bi. Roxy alikuwa na maswali mengi kichwani kuhusu maisha ya rais Xi, kama vile akiwa mtu mwenye shughuli nyingi zaidi duniani, anakabliana vipi na shinikizo za aina mbalimbali. Pia walizungumzia mambo mengine, kwa mfano mada za familia na watoto.

    Bi. Roxy alisema, rais Xi alimwuliza maswali mengi kuhusu wanyama, pia alimueleza jitihada za China katika uhifadhi wa wanyama pori. Aliona kuwa rais Xi ana nia halisi ya kuhifadhi wanyama.

    Bi. Roxy alisema, ziara ya rais Xi kwenye kituo hicho cha kuwaokoa wanyama poripia imevutia watalii wengi zaidi, watalii wengi kutoka China wamekwenda kutembelea kituo hicho.

    Bi. Roxy anaona kuwa, rais Xi ana akili, ni kiongozi anayewavutia watu wengine. Anataka kukutana naye kwa mara nyingine tena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako