• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kwa nini doriani linanuka sana?

  (GMT+08:00) 2017-10-13 19:15:25

  Doriani limesifiwa kuwa mfalme wa matunda katika Asia ya Kusini Mashariki, lakini linatoa harufu ya kipekee, ambayo baadhi ya watu wanaipenda na wengine wanaichukia. Je, harufu hiyo inatoka wapi?

  Kikundi cha kimataifa kinachoongozwa na wanasayansi wa Singapore kimetoa ripoti kwenye gazeti la Nature Genetics la Uingereza ikisema wamechambua jeni kamili za doriani, na kuthibitisha baadhi ya jeni zinazohusiana na harufu.

  Watafiti wamepima jeni za doriani aina ya Musang King, na kugundua kuwa doriani hilo lina jeni elfu 46, ambazo ni mara mbili ya jeni za binadamu.

  Kemikali muhimu inayounda harufu mbaya ya doriani ni Sulfide inayoweza kugeuka kuwa hewa. Watafiti wamegundua kuwa baadhi ya jeni zinachangamka sana wakati doriani linapoiva, na kulifanya doriani kutoa harufu kali.

  Mimea mingine pia ina jeni hizi, lakini jeni hizi zina nakala moja au mbili tu, na jeni za doriani zina nakala nne, ambazo zinalifanya kutoa Sulfide nyingi zaidi.

  Watafiti wanaona jeni hizi ni muhimu kwa doriani pori, kwani harufu kali inasaidia kuwavutia wanyama kula doriani na kueneza mbegu zake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako