• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 7 wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China wafungwa

    (GMT+08:00) 2017-10-14 20:29:51

    Mkutano wa 7 wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China umefungwa leo hapa Beijing, na kuamua kuitisha mkutano mkuu wa kamati kuu ya 19 ya chama hicho tarehe 18 mwezi huu.

    Mkutano huo umejadili na kupitisha ripoti kuhusu kazi mbalimbali za Chama cha Kikomunisti cha China, ukiona kuwa katika miaka mitano iliyopita, utekelezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango na ujenzi wa mambo ya kisasa ya ujamaa umepata mafanikio ya kihistoria. Mkutano huo pia umejumuisha na kupongeza kazi za Kamati kuu ya 18 ya Ukaguzi wa Nidhamu.

    Mkutano huo pia umechambua hali na majukumu ya hivi sasa, na kujadili kwa kina baadhi ya masuala muhimu katika hali mpya, na kufanya maandalizi ipasavyo kwa ajili ya mkutano mkuu wa kamati kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako