• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha Kikomunisti cha China chaitisha mkutano na watu wasio wanachama wake

    (GMT+08:00) 2017-10-15 18:29:43

    Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China imeitisha mkutano na watu wasio wanachama wa chama hicho, ili kusikiliza maoni na mapendekezo yao kuhusu muswada wa ripoti itakayotolewa kwenye mkutano wa 19 wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China utakaofanyika hivi karibuni.

    Rais Xi Jinping ameendesha mkutano huo akisema vyama vya demokrasia ni wenzi wa karibu wa Chama cha Kikomunisti cha China, na sera ya ushirikiano wa vyama na mashauriano ya kisiasa chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China ni moja kati ya sera za kimsingi za siasa nchini China.

    Wajumbe wa watu wasio wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China wametoa hotuba, wakiona kuwa tangu kufanyika kwa mkutano wa 18 wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, kamati hiyo ikiongozwa na rais Xi Jinping imepata mafanikio makubwa katika kusukuma mbele shughuli za ujamaa wenye umaalumu wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako