• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Riadha: Shieys Jepkosgei na Florence Chepsoi nje ya mashindano

    (GMT+08:00) 2017-10-16 08:16:40

    Wanariadha wa Kenya, Shieys Jepkosgei na Florence Jepkosgei Chepsoi wataendelea kutumikia adhabu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli katika riadha.

    Wiki iliyopita, Jopo la waamuzi wa michezo nchini Kenya liliunga mkono uamuzi wa shirika la kukabiliana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli la Kenya (ADAK) kuwa wanariadha hao walivunja sheria zinazopinga matumizi ya dawa hizo.

    Shieys alipatikana na hatia ya kutumia dawa zilizoharamishwa baada ya vipimo wakati wa mbio za kilomita 21 za Hari Sukan Negara jijini Kuala Kumpur nchini Malaysia mnamo Oktoba 8, 2016. Naye Chepsoi alishiriki shindano moja nchini Uchina mnamo Novemba mwaka 2015 baada ya kupatikana na kosa la kutumia dawa zilizoharamishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako