Naibu katibu wa chama cha Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdulla Juma Saadalla amesema chama chake kina matumaini kuwa mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China utafanyika kwa mafanikio.
Bw Saadalla amesema mwaka 2013 rais Xi Jinping wa China alifanya ziara nchini Tanzania mara baada ya kuingia madarakani, ambapo alishirikiana na aliyekuwa rais wa Tanzania Bw Jakaya Kikwete kuinua uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Amesema katika miaka 5 iliyopita, chama cha kikomunisti cha China na chama cha Mapinduzi vimeshirikiana kwa kina katika mambo ya uchumi, biashara na maendeleo ya kijamii.
Bw. Saadalla pia amesema, katika miaka 5 iliyopita, chama cha kikomunisti cha China na chama cha mapinduzi vikiwa vyama tawala, vimefanya mawasiliano kuhusu mambo ya utawala wa taifa. Amesema Chama cha Mapinduzi kinafuatilia sana mkutano mkuu wa 19 wa chama cha kikomunisti cha China, na kuutakia upate mafanikio.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |