Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China utafunguliwa tarehe 18 hapa Beijing. Profesha Yan Shuhan kutoka Chuo cha Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ambaye pia ni mtaalamu mkuu wa kikundi cha wasomi wanaoshughulikia utafiti na ujenzi wa nadharia ya Umarx amesema, mkutano huo utafanya majumuisho ya uzoefu wa miaka iliyopita, na kutunga mipango ya siku zijazo, na utafanya kazi muhimu katika mchakato wa kuendeleza shughuli za ujamaa wenye umaalumu wa China .
Katika miaka 96 tangu Chama cha Kikomunisti cha China kianzishwe, mikutano mikuu yote ya chama imefanyika katika wakati muhimu wa kihistoria. Bw. Yan amesema kazi ya kihistoria ya mikutano hiyo ni kujumuisha uzoefu wa miaka iliyopita, na kutunga mipango ya siku zaijazo.
"Chama chetu kinatilia maanani na kuwa na uhodari wa kufanya majumuisho ya uzoefu wake, kwani tunafanya kazi ambazo hazijawahi kufanywa na wengine. Kufanya majumuisho ya uzoefu ni mchakato wa kutafiti na kujaribu, ambao umetupatia kanuni nyingi. Kanuni hizo zinaweza kuelekeza kazi zetu, na kuweka msingi kwa ajili ya utungaji wa mipango yetu."
Mkutano mkuu wa 3 wa Kamati kuu ya 11 ya Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1978, uliamua kufanya ujenzi wa mambo ya kisasa ya ujamaa kuwa ni kazi kuu ya chama na serikali, na China ilianza kuingia kipindi kipya cha mageuzi na ufunguaji mlango. Katika mikutano mikuu 7 iliyofuata, ujamaa wenye umaalumu wa China uliotolewa na hayati kiongozi wa China Bw. Deng Xiaoping, umekamilika hatua kwa hatua baada ya utekelezaji, na umekuwa njia maalumu ya kujiendeleza ya China inayojulikana duniani. Bw. Yan anasema,
"Mkutano wa 14 uliofanyika mwaka 1992 ulifanya majumuisho ya hali ya utekelezaji wa sera mpya na uzoefu wa kimsingi wa miaka 14 tangu mkutano mkuu wa 3 wa Kamati kuu ya 11 ya chama ufanyike, na kutoa lengo letu la mageuzi ya uchumi ambayo ni kujenga uchumi wa soko huria wenye umaalumu wa kijamaa. Na hadi sasa bado tunaendelea na lengo hilo. Mkutano mkuu wa 16 uliofanyika mwaka 2002 ulitoa mwongozo wa kuelekea karne ya 21, na nadharia ya uwakilishi mtatu. Miaka 5 iliyopita, mkutano mkuu wa 18 ulitoa mtizamo wa maendeleo ya kisayansi, na kuuweka kwenye katiba ya chama."
Tangu mkutano mkuu wa Kamati kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China, ujamaa wenye umaalumu wa China uliingia kwenye kipindi kipya cha maendeleo, sera ya ufunguaji mlango na ujenzi wa mambo ya kisasa ya ujamaa ulipata mafanikio makubwa, na shughuli za chama na serikali zimekuwa na mabadiliko ya kihistoria. Bw. Yan amesema katika miaka 5 iliyopita, kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambayo katibu mkuu wake ni Xi Jinping inapoongoza chama na wananchi kufungua ukurasa mpya wa kujenga ujamaa wenye umaalumu wa China, ilianzisha nadharia, mawazo na mkakati mpya. Bw. Yan amesema China imepata uzoefu mkubwa tangu mkutano mkuu wa 18, ambao unastahili kujumuishwa kwa makini.
Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China utakaofanyika hivi karibuni unafuatiliwa sana na dunia nzima. Wachambuzi wanaona kuwa mkutano huo utaleta athari kubwa kwa China na kwa dunia. Bw. Yan anasema,
"Kwa nini mkutano huo unafuatiliwa sana na dunia nzima? Kwa kuwa sasa ni kipindi muhimu ya kihistoria. Sasa ni mwisho wa miaka 100 ya kwanza, tutakamilisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote hadi kufikia 2020. Sasa pia ni mwanzo wa miaka 100 ya pili, nchi yetu itatunga mipango muhimu kuhusu maendeleo ya siku za baadaye."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |