Naibu mkurugenzi wa idara ya mipango ya maendeleo ya wizara ya kilimo ya China Bw. Liu Beihua, amesema kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2016, wastani wa mapato ya wanavijiji kwenye sehemu maskini nchini China umeongezeka kwa asilimia 10.7 kwa mwaka.
Bw. Liu amesema lengo la kupunguza umaskini kupitia njia ya kukuza shughuli za viwanda ni kuwaondoa watu kwenye lindi ya umaskini, na kukuza shughuli mbalimbali ni moja ya njia za kutimiza lengo hilo. Amesema ni lazima kuwafanya watu maskini wanufaike na maendeleo ya shughuli hizo, na sio kuzingatia tu thamani ya uzalishaji na mapato ya kodi yanayotokana na shughuli hizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |