• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanahabari zaidi ya 3,000 kuripoti Mkutano Mkuu wa CPC

    (GMT+08:00) 2017-10-17 10:42:38

    Wanahabari zaidi ya 3,000 wako Beijing kuripoti Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC.

    Habari kutoka Kituo cha vyombo vya habari cha mkutano huo zinasema, jumla ya wanahabari 3,068 kutoka ndani na nje ya nchi wapo Beijing kuripoti mkutano huo. Miongoni mwao, 1,818 wanatoka mikoa ya utawala maalumu ya Hong Kong, Macao, pamoja na Taiwan na nchi mbalimbali duniani, idadi ambayo imeongezeka kwa asilimia 6.7 kuliko Mkutano mkuu wa 18 wa CPC uliofanyika miaka mitano iliyopita.

    Kwa mujibu wa kituo hicho, wanahabari wa kigeni wanatoka nchi 134 duniani, ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.6 kuliko mkutano mkuu uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako