Tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha kikomunisti cha China ufanyike mwaka 2012, kamati kuu ya chama hicho imetoa kipaumbele kwa maendeleo ya elimu, na kuendelea kuboresha usimamizi wa sekta ya elimu.
Kwa sasa elimu ya lazima ya miaka tisa kutoka shule ya msingi hadi sekondari ya chini inapatikana katika nchi nzima, na elimu ya sekondari ya juu inapatikana karibu nchi nzima.
Pia uandikishaji wa watoto kwenye vituo kabla ya chekechea umefikia asilimia 77.4 na wa elimu ya juu umefikia asilimia 42.7.
Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa mwaka 2016, hali ya kuridhika ya wanafunzi wa vyuo imefikia asilimia 92.7.
Kamati kuu cha Chama cha kikomunisti cha China pia imeamua kuhimiza mageuzi kwenye sekta ya elimu, ikiwa ni pamoja na uandikishaji wa wanafunzi, kuongeza ubora wa elimu na haki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |