Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China utafunguliwa kesho asubuhi hapa Beijing, ukiwa na ajenda tano muhimu zotakazojadiliwa kwenye mkutano huo wa siku saba, ikiwemo marekebisho ya katiba ya chama hicho.
Msemaji wa mkutano huo Bw. Tuo Zhen amesema ajenda kuu ya mkutano huo ni kusikiliza na kuthibitisha ripoti iliyotolewa na Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, kuthibitisha ripoti ya kazi iliyotolewa na Kamati ya ukaguzi wa nidhamu ya Kamati kuu ya 18 ya chama kujadili na kupitisha muswada wa marekebisho ya katiba ya Chama cha Kikomunisti cha China, kuchagua Kamati kuu ya 19 ya chama hicho, na kuchagua kamati mpya ya ukaguzi wa nidhamu ya kamati kuu ya chama hicho.
Bw. Tuo Zhen pia ameeleza kuwa wajumbe 2,280 wamethibitishwa kuwa na haki ya kuhudhuria mkutano huo, wakiwakilisha wanachama wote zaidi ya milioni 89 wa Chama cha Kikomunisti cha China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |