• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwandishi wa habari wa Jamhuri ya Watu wa Congo atarajia maendeleo mazuri zaidi ya China

    (GMT+08:00) 2017-10-17 19:56:55

    Mwandishi wa habari mwandamizi wa Gazeti la Le Potentiel la Jamhuri ya Watu wa Congo Bw. Cyprien Kapuku ambaye yupo China kuripoti Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China jana alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari amesema, mafanikio ya maendeleo ya China yamepatikana kutokana na juhudi za wachina chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, na anatarajia China itapata maendeleo mazuri zaidi baada ya mkutano huo.

    Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, utakaofanyika kuanzia kesho, ni mkutano muhimu wa China katika kipindi muhimu cha kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, na maendeleo ya Ujamaa wenye umaalumu wa China. Bw. Cyprien anaona huu pia ni mkutano muhimu wa kisiasa wenye maana ya kimataifa.

    "Mkutano huo ni muhimu kwa dunia nzima. Naona kuwa huu ni mkutano mkubwa wenye umuhimu wa kimataifa. Hii ndiyo sababu ya kuwepo kwa waandishi wa habari wapatao karibu elfu mbili kutoka nchi za nje hapa Beijing kwa ajili ya kuripoti mkutano huo. Dunia nzima itafuatilia azimio litakalotolewa kwenye mkutano huo. Tunajua sasa China ni nchi kubwa yenye nguvu ya kulinda amani ya dunia. Naamini kuwa nchi nyingine zitarekebisha sera zao za kimataifa kwa mujibu wa matokeo ya mkutano huo."

    Bw. Cyprien anaona kuwa katika miaka 5 iliyopita, China imepiga hatua kubwa katika kukuza uchumi, kuhifadhi mazingira ya asili na kupunguza umaskini, na anatarajia mafanikio makubwa zaidi yatapatikana baada ya mkutano huo.

    "Naona baada ya mkutano huo, China itapata maendeleo mazuri zaidi. mkutano huo utatoa mpango wa maendeleo ya miaka ijayo, ambao utaelekeza China kutimiza lengo la kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote kabla ya kutimia miaka 100 tangu Chama cha Kikomunisti cha China kianzishwe. Halafu itakapotimia miaka 100 tangu Jamhuri ya Watu wa China ianzishwe, China itatimiza lengo la kuijenga China iwe nchi ya kisasa ya kijamaa yenye utajiri, nguvu, demokrasia, ustaarabu na masikilizano."

    Bw. Cyprien ameeleza kuwa hivi sasa mambo ya China wanayoyajua zaidi waafrika ni kuhusu uchumi, wengi wao hawajui sera ya kisiasa ya China. Akiwa mwandishi wa habari atakayefanya mahojiano kuhusu Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Bw. Cyprien atajitahidi kujulisha sera za kisiasa za China na ubora wake kwa watu wa Afrika.

    "Nchi nyingi za Afrika zilitawaliwa na wakoloni wa nchi za magharibi. Wakati wa ukoloni, vyombo vya habari vya nchi za magharibi vilikuwa na uhasama dhidi ya nchi za ujamaa katika ripoti zao. Hivyo watu wa Afrika hawaelewi vizuri sera za kisiasa za China. Sisi waandishi wa habari wa Afrika tunapaswa kujitahidi kubadilisha hali hii. Tutawafahamisha watu wa Afrika kuhusu sera za kisiasa za China ambazo ni tofauti na walivyofikiria kupitia ripoti zetu. Sera hizo zimesababisha mafanikio ya China."

    Bw. Cyprien ameeleza kuwa katika miaka 5 iliyopita, hasa baada ya rais Xi Jinping wa China kutoa hatua za kuhimiza maendeleo ya Afrika katika mkutano mkuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyka huko Johannesburg, Afrika Kusini, uhusiano kati ya China na Afrika umeendelea kwa kasi. Nchi za Afrika zinafuatilia sana mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China. Anatarajia uhusiano kati ya pande hizo mbili utaendelezwa zaidi baada ya mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako