• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuzindua mfuko wa kuwasaidia watu walioathirika na shambulizi la kigaidi la Mogadishu

    (GMT+08:00) 2017-10-18 09:51:46

    Kenya imezindua mfuko wa kuwasaidia walioathirika na shambulizi la kigaidi lililotokea Jumamosi iliyopita mjini Mogadishu, Somalia.

    Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bibi Amina Mohamed amesema mfuko huo unalenga kuongeza rasilimali kwa ajili ya uitikiaji wa haraka na kufufua hali ya maisha. Amesema Kenya itachangia tani 11 za dawa na kutuma ndege mbili nchini Somalia kuwachukua watu waliojeruhiwa na kuwapeleka Kenya kwa matibabu.

    Habari nyingine zinasema, rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za rambirambi kwa rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia kutokana na shambulizi hilo, na kuwatakia majeruhi wapone haraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako