• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kwanza wa Kamati ya utendaji ya mkutano wa 19 wa CPC wafanyika

    (GMT+08:00) 2017-10-18 09:56:14


    Mkutano wa kwanza wa Kamati ya utendaji ya Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China ulifanyika jana mchana hapa Beijing. Rais Xi Jinping alihudhuria na kuhutubia mkutano huo.

    Mkutano huo ulioendeshwa na katibu mkuu wa mkutano mkuu Bw. Liu Yunshan ulipitisha orodha ya wajumbe 42 wa Kamati hiyo akiwemo rais Xi Jinping.

    Ajenda mbalimbali za mkutano huo zilifanyika chini ya uendeshaji wa rais Xi Jinping. Bw Liu Qibao, Meng Jianzhu, Zhao Leji na Li Zhanshu waliidhinishwa kuwa manaibu makatibu wakuu wa mkutano mkuu.

    Mkutano huo umepitisha ripoti ya ukaguzi kuhusu uwezo wa uwakilishi walionao wajumbe wanaohudhuria mkutano mkuu wa 19 wa chama, ambayo ilitolewa na kamati ya ukaguzi kwenye Mkutano mkuu wa 19 wa Chama.

    Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wajumbe 2,287 walichaguliwa baada ya kuteuliwa kutoka ngazi mbalimbali za uchaguzi kote nchini na kuidhinishwa na Kamati Kuu ya Chama cha kikomunisti cha China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako