Bw. Xi Jinping alipotoa ripoti kwenye mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China unaofanyika leo hapa Beijing, amesema katika miaka mitano iliyopita, kamati kuu ya chama imedhamiria kubadilisha hali ya kulegalega kwenye usimamizi wa chama, na kutekeleza wajibu wa kisiasa wa kusimamia nidhamu ya chama kwenye ngazi zote, hatua ambazo zimeimarisha imani na nidhamu ya wanachama, na kuendelea kukamilisha mfumo wa sheria na kanuni za chama.
Rais Xi ameona kuwa mapambano dhidi ya ufisadi katika chama, ambayo ni suala linalolalamikiwa zaidi na wananchi na pia ni tishio kubwa zaidi kwa msingi wa utawala wa chama, bila kujali ni mapapa au vidagaa, yameimarishwa na kuendelea kupiga hatua kubwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |