Katibu mkuu wa kamati kuu ya chama Bw. Xi Jinping amesema chama cha Kikomunisti cha China kimekuwa na Fikra ya Ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya, tangu mkutano wa 18 wa chama ufanyike miaka mitano iliyopita, na kuitaja kuwa ni mwongozo wa utendaji kwa chama na wananchi wa China kutimiza lengo la kustawisha taifa la China, ambao unapaswa kutekelezwa na kuendelezwa siku hadi siku.
Fikra hii imeweka lengo la kuijenga China kuwa nchi kubwa ya kisasa ya ujamaa yenye neema, demokrasia, ustaarabu na masikilizano ifikapo katikati ya karne hii, kwenye msingi wa kukamilisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora mwaka 2020.
Fikra hii inakitaka chama kishikilie wazo la kujiendeleza linalozingatia kwa ajili ya wananchi, kuendelea kuhimiza wananchi wapate maendeleo kwa pande zote na kupata maisha bora kwa pamoja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |