Katika ripoti ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Bw. Xi Jinping amesema Chama cha Kikomunisti cha China kinapoongoza nchi ya kijamaa yenye watu zaidi ya bilioni 1.3, kinatakiwa kuimarisha uwezo wa utawala katika pande zote, ambao ni pamoja na uwezo wa kujifunza, na uwezo wa uongozi wa kisiasa, uwezo wa kufanya mageuzi na uvumbuzi, uwezo wqa kujiendeleza kwa njia ya kisayansi, uwezo wa kutawala kwa mujibu wa sheria, uwezo wa kushughulikia mambo ya umma, uwezo wa kutekeleza kazi mbalimbali kwa makini, na uwezo wa kukabiliana na changamoto. Amesisitiza kuwa chama tawala kinatakiwa kuwa na wazo la kimkakati, la kufanya uvumbuzi, la kuchanganua katika kutawala kwa mujibu wa sheria, na la kutokiuka msingi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |