• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano mkuu wa 19 wa CPC wasisitiza kuwa China kamwe haitafuti umwamba na kujipanua

    (GMT+08:00) 2017-10-18 12:49:31

    Katibu mkuu wa Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Xi Jinping alipotoa ripoti kwenye ufunguzi wa mkutano mkuu wa 19 wa chama uliofanyika leo hii hapa Beijing, amesisitiza kuwa China siku zote inafuata kithabiti sera za amani za kidiplomasia za kujiamulia na kujitawala, itaheshimu haki ya watu wa nchi mbalimbali kuchagua njia ya kujiendeleza, itatetea na kulinda haki na usawa wa kimataifa, na kupinga vitendo vya kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine na kuzionea nchi dhaifu.

    Bw. Xi amesisitiza kuwa China kamwe haitajiendeleza kwa njia ya kuharibu maslahi ya nchi nyingine, na kamwe haitaacha maslahi yake halali.

    Amesema China inatekeleza sera ya ulinzi ya kujilinda, na kusisitiza kuwa maendeleo ya China hayatatishia nchi nyingine, na kamwe haitafuti umwamba na kupanua ardhi yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako