• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi Jinping atangaza Ujamaa wenye umaalumu wa China kuingia kipindi kipya

    (GMT+08:00) 2017-10-18 18:13:23

    Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China umefunguliwa leo hapa Beijing. Kwa niaba ya kamati kuu ya 18 ya chama hicho, Bw. Xi Jinping amehutubia mkutano huo akitangaza kuwa, kwa kufuata itikadi ya Ujamaa wenye umaalumu wa China katika kipindi kipya, Chama cha Kikomunisti cha China kitaongoza wananchi wa China kukamilisha kazi ya kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

    Katika miaka 5 iliyopita, Chama cha Kikomunisti cha China kimeimarisha uongozi wake, na kutekeleza mawazo na mikakati mingi mipya ya utawala. Hivi sasa China inachangia asilimia 30 ya ongezeko la uchumi wa dunia, na kufanikiwa kuwasaidia watu zaidi ya milioni 60 kuondokana na umaskini. Bw. Xi amesema maendeleo ya China yamefungua ukurasa mpya wa kihistoria.

    Mkutano mkuu wa 12 wa Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika zaidi ya miaka 30 iliyopita ulitoa uamuzi wa kujenga Ujamaa wenye umaalumu wa China kwa mara ya kwanza, na Ujamaa wenye umaalumu wa China ulianza kuwa kiini cha nadharia na majaribio ya utawala wa chama baada ya utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Mkutano huu wa 19 umerithi nia ya awali, na pia kuiendeleza na kufanya uvumbuzi, kwa kutangaza Ujamaa wenye umaalumu wa China umeingia katika kipindi kipya. Bw.Xi anasema,

    "Nia ya Ujamaa wenye umaalumu wa China katika kipindi kipya imedhihirisha umuhimu wa kushikilia na kuendeleza Ujamaa wenye umaalumu wa China, na jukumuu kuu ni kutimiza mambo ya kisasa ya kijamaa na kustawisha upya taifa la China, baada ya kumaliza kazi ya kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, China itaendelezwa na kuwa nchi nzuri ya kisasa ya kijamaa yenye utajiri, nguvu, demokrasia, ustaarabu na masikilizano kwa hatua mbili ifikapo katikati ya karne hii. Pia imedhihirisha kuwa katika kipindi kipya, changamoto kuu inayoikabili jamii yetu ni pengo kati ya mahitaji ya watu ya kuwa na maisha bora na kutokuwa na uwiano wa maendeleo ya kutosha, hivyo tunapaswa kushikilia wazo la ya kujiendeleza kwa ajili ya wananchi wetu, kuhimiza maendeleo ya watu katika kila upande, na kupata maisha bora kwa wananchi wote."

    Miaka 5 iliyopita, mkutano mkuu wa 18 ulidhihirisha malengo mawili ya miaka 100, ambayo ni kukamilisha kazi ya kujenga jamii yenye maisha bora hadi kufikia mwaka 2021 wakati itakapotimia miaka 100 tangu Chama cha Kikomunisti cha China kianzishwe, na kuijenga China iwe nchi ya kisasa ya kijamaa mwaka 2049 wakati itakapotimia miaka 100 tangu Jamhuri ya Watu wa China ianzishwe. Wakati China itakapotimiza lengo la kwanza, na kuanza kutimiza lengo la pili, Bw. Xi ametoa mpango wa kimkakati kwenye ripoti yake.

    "Kwa kuchambua hali za ndani na duniani na mazingira ya maendeleo ya nchi yetu, tunaweza kupanga kazi katika vipindi viwili kati ya mwaka 2020 na katikati ya karne hii. Kipindi cha kwanza ni kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2035, baada ya kumaliza kazi ya kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, tutaijenga China kuwa nchi ya kisasa ya kijamaa kwa kutumia miaka 15. Kipindi cha pili ni kuanzia mwaka 2035 hadi katikati ya karne hii, baada ya kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya kijamaa, tutaendelea kuiendeleza kuwa nchi nzuri ya kisasa ya kijamaa yenye utajiri, nguvu, demokrasia, ustaarabu na masikilizano."

    Ukilinganishwa na mpango wa zamani, ripoti iliyotolewa kwenye mkutano wa 19 imerekebisha lengo litakalotimizwa ifikapo katikati ya karne hii, na kuongeza maneno ya "vizuri na nguvu", hali ambayo inamaanisha kuwa Chama cha Kikomunisti cha China kinatilia maanani uhifadhi wa mazingira, na pia kimeinua kiwango cha lengo hilo.

    Alipozungumzia sera za kidiplomasi za China, Bw. Xi amesisitiza kuwa Chama cha Kikomunisti cha China siku zote kinaona kutoa mchango zaidi kwa ajili ya binadamu wote kuwa ni jukumu lake. China itashikilia njia ya kujiendeleza kwa amani, kuhimiza kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, kutekeleza kithabiti sera za kidiplomasi za amani za kujitawala na kujiamulia, kuendeleza uhusiano wa kiwenzi kote duniani kwa hatua madhubuti, kupanua maslahi ya pamoja na nchi mbalimbali, kushikilia sera ya kimsingi ya taifa ya mageuzi na ufunguaji mlango, kushikilia kufanya ujenzi kwa kufungua mlango, kusukuma mbele kwa hamasa ushirikiano wa kimataifa wa kanda moja na njia moja, na kushikilia mawazo ya utawala wa kimataifa yanayojengwa kwa pamoja baada ya mazungumzo na kuweza kunufaisha pande zote.

    Katika miaka 5 iliyopita, pande zote nchini China na za nchi za nje zimekipongeza Chama cha Kikomunisti cha China kwa mafanikio ya kushughulikia mambo ya ndani ya chama. Akiwa kiongozi wa chama, Bw.Xi anasema,

    "Wananchi wanachukia zaidi ufisadi, ambao ni tishio kubwa zaidi dhidi ya chama chetu. Kama tunashikilia nia thabiti ya kupambana na vitendo vya ufisadi kwa njia mbalimbali ili kuhakikisha maofisa na serikali yetu inaondokana na vitendo hivyo, tutaweza kudumisha utawala wetu."

    Bw. Xi ameeleza kuwa, Chama cha Kikomunisti cha China kinapaswa kuendelea kuwaadhibu watu wanaopokea rushwa pamoja na wale wanaotoa rushwa, kukinga kwa hatua thabiti kuwepo kwa kundi la maslahi katika chama, na kuwasaka na kuwashtaki mafisadi bila kujali wametorokea wapi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako