• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Hispania yasema hali ya kujiendesha ya Catalan inaweza kusimamishwa

  (GMT+08:00) 2017-10-18 19:24:12

  Waziri mkuu wa Hispania na naibu wake, wamesema serikali ya Hispania imejiandaa kutumia kipengeleza cha 155 cha katiba kusimamisha hali ya kujiendesha ya jimbo la Catalan.

  Serikali ya waziri mkuu wa nchi Bw. Mariano Rajoy imetishia kuchukua hatua hiyo kama kiongozi wa Catalan Bw. Carles Puigdemont hatatoa maelezo kabla ya kesho saa nne asubuhi, kama serikali yake imetangaza kujitenga au hapa, na kama imetangaza kujitenga iondoe tangazo hilo.

  Naibu waziri Mkuu Bw. Soraya Saenz naye amesema kama Bw. Puidgemont hajatoa maelezo katika muda huo, basi kipengele cha 155 cha katiba kitatumika.

  Patashika linaloendelea linatokana na kura za maoni kuhusu eneo la Catalan kujitenga na Hispania, zilizopigwa Oktoba mosi mwaka huu. Mahakama ya katiba ya Hispania ilitangaza kuwa upigaji kura huo ni kinyume na sheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako