• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ofisa wa IEBC ajiuzulu kabla ya uchaguzi wa urais kufanyika tena nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2017-10-18 20:32:17

  Ofisa wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Kenya IEBC Bibi Roselyn Akombe amejiuzulu, huku akitoa wito kusimamisha uchaguzi wa urais utakaofanyika wiki ijayo.

  Kamishna wa tume hiyo Bi Akombe ametoa taarifa kutoka New York ikisema, tume hiyo ya usimamizi inatakiwa kutoa maelezo, kwa sababu uchaguzi unaopangwa kufanyika Oktoba 26 hauwezi kufika matarajio ya msingi ya uchaguzi wenye uaminifu.

  Bi Akombe ameeleza msimamo wa chama uliochukuliwa na wenzake, huku akisema kuwa ni vigumu kuendelea kuhudhuria mikutano wa wajumbe wote, ambayo makamishna wamekuwa tayari kupiga kura kufuata vyama vyao, badala ya kujadili masuala yanayowakabili.

  Bi Akombe alitakiwa kwenda kuchunguza uchapishaji wa karatasi za kupigia kura huko Dubai, lakini alienda makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako