• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Somalia aahidi kuwa Somalia itajibu vikali shambulizi la kigaidi lililotokea jumamosi

    (GMT+08:00) 2017-10-19 09:01:07

    Rais Mohamed Abdulahi Mohamed wa Somalia amesema atajibu vikali shambulizi la kigaidi lililotokea jumamosi na kulionya kundi la Al Shabaab kuwa litaadhibiwa vikali kutokana na shambulizi hilo.

    Akiwahutubia mamia ya watu waliokusanyika katika uwanja mjini Mogadishu, Rais Mohamed amesema shambulizi hilo limeonyesha kuwa huko nyumba hakukuwa na hatua kali dhidi ya kundi hilo. Amewataka wananchi wa Somalia wawe na umoja na kuwataka vijana wa nchi hiyo kuilinda nchi yao.

    Idara za usalama zimesema mpaka sasa zimekamatwa watuhumiwa watatu wa shambulizi hilo, ambalo hadi sasa limesababisha vifo vya watu zaidi ya 303.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako