Kamishna wa kamati ya Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya usalama Bw Jullian King amesema Umoja wa Ulaya utatumia Euro milioni 118.5 kuirekebisha baadhi ya miji barani Ulaya, ili kupunguza hatari ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi.
Bw Jullian amesema nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zitaweka sera kali ili kuimarisha udhibiti wa uuzaji wa bidhaa za kemikali, na kujenga uwezo wa kukabiliana na matishio ya mashambulizi ya kikemikali, kibiolojia na kinyuklia.
Amesema marekebisho hayo ni pamoja na kupanga upya sehemu za umma, taa na mifumo ya kukabiliana na hali ya dharura mijini, ili kuifanya miji hiyo iwe salama zaidi.
Ameongeza kuwa jumuiya ya kimataifa bado inakabiliwa na changamoto kubwa katika kupamabana na ugaidi, na bado ipo uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi huko Ulaya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |