• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jimbo la wakurdi la Iraq laahirisha uchaguzi wa wabunge na mwenyekiti

    (GMT+08:00) 2017-10-19 09:44:53

    Tume ya uchaguzi na kura za maoni ya jimbo la wakurdi nchini Iraq imesema kazi ya maandalizi ya uchaguzi wa wabunge na mwenyekiti jimbo la wakurdi uliopangwa kufanyika tarehe mosi mwezi ujao imesimamishwa, na upigaji kura wa uchaguzi huo utaahirishwa.

    Taarifa iliyotolewa na tume hiyo imesema kutokana na hali ya wasiwasi kwenye jimbo hilo na kuchelewa kwa kazi ya kuandikisha wagombea, kazi ya maandalizi ya uchaguzi huo itasimamishwa hadi uamuzi mpya utakapotolewa na bunge la jimbo hilo.

    Mwenyekiti wa jimbo la wakurdi Bw Massoud Barzani alisaini amri tarehe 19 mwezi Juni, akitoa agizo la kufanya uchaguzi wa wabunge na mwenyekiti Novemba mosi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako