Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC ulifunguliwa jana hapa Bejing. Kwa niaba ya Kamati kuu ya 18 ya CPC, Bw. Xi Jinping alitoa ripoti ya Kukamilisha Kujenga Jamii yenye Maisha Bora kwa Pande zote, na Kupata Mafanikio Makubwa ya Ujamaa wenye Umaalumu wa China katika Kipindi Kipya. Wajumbe wanaohudhuria mkutano huo wanajadili ripoti hiyo, na kuona imedhihirisha mwelekeo wa kazi katika muda mrefu wa baadaye.
Bw. Xi Jinping kwenye ripoti hiyo ameeleza kuwa, baada ya kufanya juhudi za muda mrefu, Ujamaa wenye Umaalumu wa China umeingia katika kipindi kipya, hii ni alama mpya ya kihistoria ya maendeleo ya nchi yetu. Mjumbe Shi Taifeng, ambaye ni katibu wa kamati ya chama ya mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia, anaona mvuto mkubwa zaidi wa ripoti hiyo ni kwamba imeeleza nia ya kujenga Ujamaa wenye umaalumu wa China katika kipindi kipya, ambayo itakuwa mwongozo wa juhudi za kustawisha upya taifa la China.
"Nia hii imejibu kwa kina maswali muhimu ya kuendeleza ujamaa wenye umaalumu wa China wa aina gani katika kipindi kipya, na namna ya kushikilia kuutekeleza, na maswali ya kimsingi ya malengo, kazi na mipango ya jumla ya kushikilia na kuendeleza Ujamaa wenye Umaalumu wa China katika kipindi kipya, na mwelekeo, njia, injini, hatua za kimkakati, mazingira ya nje na uhakikisho wa kisiasa katika kuuendeleza."
Bw. Xi kwenye ripoti yake pia amesema China itaongeza nguvu ya kuunga mkono sehemu zilizofuatiliwa zaidi za sehemu zenye wapigania wazee na sehemu za makabila madogomadogo, sehemu za mbali za mipaka na zile maskini kuharakisha kujipatia maendeleo, na kuimarisha hatua za kusukuma mbele maendeleo ya sehemu za magharibi. Mjumbe Shen Zuoquan, ambaye ni katibu wa kamati ya chama ya mji wa Wuzhong ya mkoa wa Ningxia amesema, mji wa Wuzhong ni sehemu yenye watu maskini iliyokuwa makazi ya wanamapinduzi. Kuanzia mwaka 2012 hadi 2016, mji huo ulipunguza umaskini kwa watu elfu 95.
"Hadi kufikia mwaka 2016, mjini kwetu kulikuwa na vijiji maskini 103, na watu maskini laki 1.1. Idadi hiyo inachukua asilimia 27 ya watu maskini mkoani Ningxia. Tutatekeleza kwa makini mpango na matakwa mapya yaliyotolewa na mkutano mkuu wa 19, na kuharakisha hatua za kuhimiza maendeleo katika sehemu zenye umaskini, kushinda kazi ngumu na kuendeleza watu, na kuondoa kihalisi umaskini kupitia maendeleo ya sehemu."
Ripoti ya Bw. Xi pia imetaja utekelezaji wa mkakati wa kustawisha vijiji, na kuona kuwa masuala ya kilimo, vijiji na wakulima ni masuala muhimu ya kitaifa, hivyo yanapaswa kuchukuliwa kuwa moja ya kazi muhimu zaidi za chama chetu. Mjumbe Yang Fengji ambaye ni katibu wa kamati ya chama ya kijiji cha Tianbiao cha wilaya inayojiendesha ya kabila la Walii ya Baisha ya mkoa wa Hainan amesema, kusoma ripoti iliyotolewa na Bw. Xi kumemfanya awe na imani na nia zaidi katika kuhimiza wanakijiji wake kupata maendeleo.
"Nimetambua kuwa katika ripoti ya rais Xi, kuna sera nyingi za kuimarisha kilimo na kuwanufaisha wakulima. Kwa mfano ameahidi kurefusha muda wa kukodi mashamba vijijini kwa zaidi ya miaka 30, na ahidi hiyo itaondoa kabisa wasiwasi wetu moyoni."
Ripoti iliyotolewa na Bw. Xi kwenye mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China imesema, chama hicho kinapaswa kushikilia kithabiti kupata maendeleo kuwa kazi yake ya kwanza, kushikilia kukomboa na kuendeleza nguvu za uzalishaji, na kushikilia mwelekeo wa mageuzi ya soko huria la kijamaa, ili kuhimiza uchumi kupata maendeleo endelevu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |