• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Ardhi isiyotumika kulipiwa ushuru

    (GMT+08:00) 2017-10-19 18:01:56

    Rais wa benki ya maendeleo ya Afrika Akinwumi Adesina amependekeza kulipishwa kodi ya juu kwa ardhi inayomilikiwa na watu ama mashirika binafsi ambayo haitumiki.

    Adesina anasema bara la Afrika litatakiwa kuhakikisha lina uwezo wa kuwalisha watu zaidi ya bilioni 9 kufikia mwaka 2050.

    Akiongea kwenye warsha ya masuala ya chakula ,amesema ardhi ambazo hazitumiki zinatakiwa kufanyiwa kilimo cha chakula cha biashara na matumizi ili kupunguza ukosefu wa chakula.

    Bara la Afrika lina miliki zaidi ya asilimia 65 ya ardhi ya rotuba ya kilimo na katika miaka ijayo nchi za magharibi zitategemea pakubwa bara hili kwa chakula.

    Kwa sasa takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 300 barani Afrika hawana chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako