• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China aitaka jumuiya ya kimataifa ishirikiane kutatua suala la Palestina

    (GMT+08:00) 2017-10-19 18:30:40

    Kaimu balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao janakatika mkutano wa majadiliano wa baraza la usalama kuhusu hali ya Mashariki ya Kati na suala la Palestina aliitaka jumuiya ya kimataifa ishirikiane kutatua suala la Palestina.

    Bw. Wu Haitao amesema suala la Palestina lipo kwa miaka mingi na ni kiini cha suala la Mashariki ya Kati. Kutatua suala la Palestina kwa njia ya mazungumzo kunalingana na maslahi ya msingi ya watu wa Palestina na Israel, na kunasaidia kuleta amani na utulivu wa sehemu hiyo.

    Bw. Wu Haitao amesema inafaa kuhimiza mchakato wa kisiasa wa kutatua suala hilo kwenye msingi wa mpango wa nchi mbili. China itaendelea kuunga mkono mpango huo, na kufanya juhudi pamoja na pande mbalimbali ili kuhimiza mchakato wa kutatua suala la Palestina kwa njia ya kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako