• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Askari 43 wa Afghanistan wauawa na kundi la Taliban kwenye kambi yao

  (GMT+08:00) 2017-10-19 18:47:06

  Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imetoa taarifa ikisema askari 43 wa jeshi lake wameuawa na wengine tisa kujeruhiwa kwenye shambulizi lililofanywa na waasi wa Taliban kwenye wilaya ya Maywand mkoa wa Kandahar.

  Taarifa hiyo imefafanua kuwa kundi la waasi lilitumia magari mawili ya vikosi vya usalama yaliyosheheni mabomu na kushambulia kambi ya jeshi la taifa ya Afghanistan ya Chishmo huko Maywand, shambulizi ambalo lilipelekea mapambano yaliyosababisha vifo kwa pande zote mbili na baada ya mapambano kumalizika askari sita hawakujulikana walipo.

  Hata hivyo msemaji wa kundi la Taliban, amedai kuwa waasi wamewaua askari 60 huko Maywand. Kwa mujibu wa taarifa waasi kumi pia wameauwa kwenye shambulizi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako