Wanahabari watano kutoka nchi za Afrika zikiwemo Sudan, Kenya, Nigeria, Tanzania na Afrika Kusini jana walihudhuria mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China na kusikiliza hotuba iliyotolewa na rais Xi Jinping wa China Wanahabari hao wote wanaona kuwa nchi za Afrika zinatakiwa kujifunza uzoefu wa China.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari cha Sudan Bw. Aslsadig Ibrahim amesema, ameandika makala inayoitwa "Chama cha CPC kina mambo mengi tunayotaka kujifunza" ikihimiza Sudan kujifunza uzoefu wa China katika uchumi, maisha ya umma na usimamizi makini wa chama.
Katibu mkuu wa kamati ya vyombo vya habari ya Tanzania Bw. Kajubi Mukajangra amesema, hotuba ya rais Xi imempatia kumbukumbu zaidi kwenye mambo ya kupunguzaumaskini na kupambana na ufisadi.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanahabari la Kenya Bw. Leonard Kwayera anaona kuwa kuwaelimisha raia kuhusu utambuzi na urithi wa utamaduni wa kikabila ni muhimu sana. Amesema, ingawa China ilikumbwa na vita na uvamizi wa maadui wa kigeni, lakini wachina wamelinda lugha na utamaduni wao, ambayo imeweka msingi thabiti wa kiutamaduni kwa maendeleo ya kasi ya China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |