• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Rwanda lalaani ripoti ya shirika la Human Rights Watch

    (GMT+08:00) 2017-10-20 09:12:19

    Bunge la Rwanda limelaani ripoti isiyoendana na hali halisi iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, ambayo inalenga kuidhalilisha Rwanda.

    Ripoti hiyo iliyotolewa tarehe 13 Julai inasema kikosi cha usalama cha Rwanda kiliwaua wahalifu 37 wanaotuhumiwa kuwa na makosa madogo katika mkoa wa magharibi mwa Rwanda kati ya mwezi Julai mwaka 2016 hadi mwezi Machi mwaka 2017.

    Tume ya taifa ya haki za binadamu ya Rwanda ijumaa iliyopita ilipinga ripoti hiyo, na kusema imeandaliwa kwenye msingi wa habari za kutungwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako