Mjumbe wa Mkutano mkuu wa 19 wa chama cha kikomunisti cha China ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, ripoti ya Mkutano mkuu wa 19 wa chama cha kikomunisti cha China inaleta utulivu kwa hali ya kimataifa yenye sintofahamu, na kuingiza msukumo mkubwa kwa ajili ya jamii ya binadamu kutafuta mustakabali mzuri.
Bw. Wang Yi amesema, ripoti muhimu aliyoitoa katibu mkuu wa chama Bw. Xi Jinping kwenye Mkutano mkuu wa 19 CPC ni ilani ya kisiasa ya wanachama wa chama cha kikomunisti cha China inayotangazia dunia nzima kuwa ujamaa wenye umaalumu wa China umeingia katika zama mpya, ambayo si kama tu itakubaliwa na wanachama na wananchi wote, bali pia itafuatiliwa na jumuiya ya kimataifa, kuzifanya nchi mbalimbali duniani zifahamu kwa usahihi na kwa uundani majukumu mapya ya kihistoria ya wanachama wa chama cha kikomunisti cha China, pamoja na mustakabali mpya wa ujamaa wenye umaalumu wa China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |