• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold Corporation zafikia makubaliano

    (GMT+08:00) 2017-10-20 19:54:17

    Rais John Magufuli wa Tanzania amesema kufikiwa makubaliano kati ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold Corporation ni mwanzo mzuri na kwamba nchi yake inachukua mwelekeo ambao haujawahi kuwekwa kote barani Afrika katika udhibiti wa rasilimali zake.

    Rais Magufuli alisema hayo katika ikulu ya Dar es salaam wakati wa kusainiwa kwa makubaliano baada ya Kamati maalumu ya mazungumzo baina ya timu ya wataalamu wa Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold Corporation kukamilika.

    Kwenye makubaliano hayo, kampuni ya Barrick imekubali kulipa Dola za Marekani milioni 300 kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kupitia biashara ya kampuni hiyo.

    Magufuli ameongeza kuwa kampuni hiyo pia imekubali kuanzia sasa Tanzania itakuwa ikipata nusu ya faida ya biashara ya kampuni hiyo ya madini ya dhahabu sambamba na kumiliki hisa kwa asilimia 16. Mbali na kulipa faida na nchi kumiliki hisa hizo, rais Magufuli amesema kampuni hiyo pia itaendelea kulipa kodi nyingine kama kawaida zikiwemo za halmashauri pamoja na menejimenti ya kampuni hiyo itaundwa kwa kuwahusisha pia watanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako