• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kura ya maoni yaonesha wateja wana imani na benki ya Equity ya Kenya

    (GMT+08:00) 2017-10-20 19:54:40

    Kura ya maoni inaonesha kuwa watu wengi wana imani zaidi na benki ya Equity ya Kenya. Kwa mujibu wa kura ya maoni iliyofanywa na shirika la GeoPoll Straw miezi miwili iliyopita, jumla ya watu 2825 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini waliojiwa walisema kilichowavutia zaidi kwenye benki hiyo ni kurahisishwa kwa mchakato wa kupata mikopo. Ya pili ilikuwa ni benki ya KCB huku benki ya ushirika yaani cooperative ikichukua nafasi ya tatu. Wakati huo huo chama cha mabenki nchini Kenya kimesema msukosuko wa kisiasa nchini humo unaendelea kuathiri biashara za benki nchini humo. Kwa mujibu wa mkuu wa chama hicho Bw Habil Olaka, wateja wengi wameshindwa kwenda kuchukua fedha za mkopo walioomba wakisema wameshindwa kujua watakavyozitumia fedha hizo wakati huu ambapo joto la kisiasa linaonekana kupanda. Habil amesema hivi sasa fedha nyingi za mikopo iliyoidhinishwa bado ziko kwenye benki zikisubiri kuchukuliwa na wateja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako