• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuimarisha mawasiliano ya utamaduni ni njia muhimu ya kuhimiza maelewano kati ya wananchi wa China na nchi nyingine

    (GMT+08:00) 2017-10-21 16:42:31

    Wajumbe kutoka sekta za utamaduni na sanaa wanaohudhuria mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China jana wamefanya mawasiliano ya moja kwa moja na waandishi wa habari wa nchini na nje.

    Mjumbe wa wa kuhudhuria mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China kutoka Redio China Kimataifa Bw. Xia Yongmin amesema, utamaduni ni njia muhimu ya kuhimiza maelewano kati ya wananchi wa China na nchi nyingine, ambao pia unafaa kuenezwa nje. Miaka kadhaa iliyopita, Redio China Kimataifa ilifanya shughuli mfululizo za mawasiliano ya utamaduni ikiwemo tafsiri za filamu na tamthilia za China kwa lugha za kigeni, na kuhimiza mawasiliano ya utamaduni kati ya China na nchi nyingine mbalimbali. Anasema,

    "Kwa mfano, Redio China Kimataifa na televisheni ya Leo Russia ziliandaa kwa pamoja shughuli za Njia ya Hariri kati ya China na Russia, na Redio China Kimataifa pia iliandaa shughuli mfululizo za ziara ya watu maarufu wa nchi za kando ya Njia ya Hariri nchini China. Tuliunda kikundi cha waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya nchi tofauti, ambacho kilielewa desturi, hali ya maendeleo ya jamii na uchumi, na utamaduni wa nchi tofauti. Kuhimiza maelewano kati ya wananchi wa nchi mbalimbali kwa kupitia ripoti za vyombo vya habari, hii ndiyo majukumu ya vyombo vya habari, pia ni njia muhimu ya kuhimiza mawasiliano ya utamaduni."

    Akizungumzia mawasiliano ya utamaduni kati ya nchi za "Ukanda mmoja na Njia moja", Bw. Xia amesema nchi hizo zina utaratibu tofauti wa siasa, njia tofauti za maendeelo na desturi na mila tofauti, hivyo ni kawaida kuwepo kwa ukosefu wa maelewano kati yao. Msingi wa urafiki kati ya nchi ni urafiki kati ya wananchi wao, na kuimarisha mawasiliano ya utamaduni ni njia muhimu ya kuhimiza urafiki kati ya wananchi wa nchi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako