Kwenye ripoti ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, rais Xi Jinping wa China ameeleza mkakati wa kuharakisha mageuzi ya utaratibu wa ustaarabu wa kiikolojia, kuhimiza kazi ya kujipatia maendeleo bila kusabbisha uchafuzi na kujenga China yenye mazingira mazuri. Wachina wengi katika nchi za nje wamesema, mazingira mazuri bila uchafuzi ni utajiri, kujenga ustaarabu wa kiikolojia ni majukumu makubwa ya wachina.
Bi. Chen Xueqin anayeishi nchini Marekani amesema, rais Xi Jinping ameeleza mwelekeo wa maendeleo, China haiwezi kuharibu mazingira ya asili ili kupata maendeleo. Na ana imani kuwa chini ya uongozi wa rais Xi Jinping, mazingira ya asili nchini China yataboreshwa siku hadi siku, na China itapata mafanikio makubwa katika kupunguza matumizi ya nishati na utoaji wa uchafu kwenye sekta ya viwanda.
Naibu mkurugenzi wa shirikisho la wachina kutoka Kaskazini Mashariki mwa China wanaoishi nchini Zambia Bw. Liu Heling amesema, serikali ya China ilichukua hatua mfululizo za kurekebisha muundo wa uchumi, ili kuboresha mazingira ya maisha ya wachina wakati wanapokuza uchumi. China ilijiunga rasmi na Makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa mwaka jana, na jambo hili limeonesha kuwa, China imeanza kufuata njia ya kujiendeleza kwa kukuza nishati safi na shughuli za teknolojia za juu badala ya kutumia nishati nyingi na kuleta uchafuzi mwingi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |