• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwango cha maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto nchini Tanzania chapungua hadi 7.6%

    (GMT+08:00) 2017-10-23 08:48:01

    Mkurugenzi wa huduma za kinga dhidi ya magonjwa katika wizara ya afya ya Tanzania Bi. Neema Rusibamayila amesema kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kimepungua kutoka asilimia 21 ya mwaka 2009 hadi kukufikia asilimia 7.6 ya mwaka jana. Akiiarifu kamati ya bunge kuhusu UKIMWI mjini Dodoma, Bi. Rusibamayila amesema wizara yake inatekeleza hatua mbalimbali za uingiliaji ili kupunguza maambukizi mapya kutoka mama kwenda kwa watoto, na lengo la Tanzania ni kupunguza kiwango hicho hadi asilimia 0.16 kati ya vizazi elfu moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako