• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Misri avitaka vyombo vya usalama kuwasaka magaidi waliowashambulia askari

    (GMT+08:00) 2017-10-23 09:13:20

    Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri amevitaka vyombo vya usalama kujitahidi kuwasaka wahusika wa shambulizi la kigaidi lililosababaisha vifo vya askari 16 mkoani Giza.

    Akiongea na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo wakiwemo waziri wa ulinziBw Sedqi Sobhi, Waziri wa mambo ya ndani Magdy Abdel Ghaffar, na Mkuu wa shirika la ujasusi Khaled Fawzi, rais Sisi ametaka kuimarishwa kwa juhudi za usalama na kijeshi ili kuzuia washambuliaji kupenya kwenye mipaka ya nchi hiyo. Pia amesisitiza kuwa Misri itaendelea kupambana na ugaidi na kukabiliana na wote wanaofadhili ugaidi.

    Juzi wizara ya mambo ya ndani ilitangaza kuwa askari 16 wameuawa na mmoja hajulikani alipo, baada ya magaidi kufanya mashambulizi Ijumaa katika mkoani Giza karibu na mji wa Cairo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako