• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yazitaka Saudi Arabia na Iraq zishirikiane kulinda usalama wa kikanda

    (GMT+08:00) 2017-10-23 09:27:36

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson ambaye yuko ziarani nchini Saudi Arabia jana amesema, Marekani inatumai kuwa Saudi Arabia na Iraq zikiwa nchi mbili kubwa za Mashariki ya Kati zitashirikiana kulinda usalama na utulivu wa kanda hiyo.

    Bw. Tillerson jana amehudhuria mkutano wa kwanza wa kamati ya uratibu kati ya Saudi Arabia na Iraq unaoendeshwa kwa pamoja na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz Al Saud na waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abad. Bw. Tillerson amesema kuwa, nchi hizo mbili kufanya mkutano huo kunaonyesha kuboreshwa kwa uhusiano kati yao, na mustakabali wa ushirikiano kati yao ni mkubwa. Amesema Marekani imefanya maandalizi kwa ajili ya kutoa msaada na uungaji mkono kwa nchi hizo mbili kuboresha zaidi uhusiano na ushirikiano kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako