• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNAMID yapunguza idadi ya askari Darfur

    (GMT+08:00) 2017-10-23 09:45:30

    Tume ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika eneo la Darfur UNAMID imetangaza kupunguza idadi ya askari huko Darfur nchini Sudan.

    Kufuatia azimio namba 2363 lililotolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, askari 1,440 na polisi 240 wameondoka kutoka kwenye sehemu hiyo.

    Msemaji wa mwakilishi maalumu wa pamoja wa UNAMID Bw. Ashraf Eissa amesema, tangu mchakato wa upangaji mpya wa tume hiyo uzinduliwe, batalioni mbili kutoka Nigeria na Pakistan zenye askari 1,400, pamoja na vikosi viwili vya polisi kutoka Bangladesh na Senegal vyenye polisi 240 wamepunguzwa na kuondoka kwenye eneo hilo.

    Bw. Eissa amethibitisha kuwa kipindi cha kwanza cha mchakato wa upangaji mpya kinachoendelea, kinatarajiwa kumalizika mwezi wa Januari mwaka 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako